UCHUNGUZI : INSTAGRAM HUARIBU AKILI ZA VIJANA.

Instagram imeorodheshwa kuwa mtandao wa kijamii
ambao una madhara zaidi kwa afya ya kiakili ya vijana.
Katika utafiti uliofanyiwa nchini Uingereza, vijana 1,479 wa
miaka kati ya 14 na 24 waliombwa kueleza utathmini wao
kuhusu mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kuzingatia
wasiwasi, mfadhaiko, upweke, dhuluma na sifa za kimwili.

Instagram ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na madhara zaidi.

Instagram hujiuza kama jukwaa salama na la kusaidia
vijana.

Mashirika ya hisani kuhusu afya ya kiakili yametoa wito
kwa kampuni kuimarisha usalama wa watu wanaotumia
mitandao ya kijamii.

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Royal Society for
Public Health unasema mitandao ya kijamii inafaa
kutambua watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa
kupitiliza na pia wale wenye matatizo ya kiakili.

Instagram husena huwa ina huduma na habari za
kuwasaidia watu kukabili wanaotekeleza dhuluma na pia
hutahadharisha watu kabla ya kutazama ujumbe, picha au
video zenye madhara.
Inakadiriwa kwamba 90% ya vijana hutumia mitandao ya
kijamii, na hivyo ndio huathirika zaidi.

No comments