SOKA : YAYA TOURE APEWA MKATABA NA MANCHESTER CITY

Kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure anakaribia kupata
mkataba mpya katika klabu yake anayochezea hivi sasa
ya Manchester City.

Toure alionekana kama hana umuhimu tena klabuni hapo
baada ya kuachwa nje katika kikosi kilichocheza michuano
ya Ulaya na hakucheza michuano ya ligi ya England mpaka
mwezi Novemba.
Lakini kadri siku zilivyokwenda alianza kuwa na umuhimu
klabuni hapo na baadaye kurejea tena kuwa muhimuli wa
timu hiyo.


Wakati huo huo Guardiola amemtaja mlinzi wake wa kulia
Pablo Zabaleta kama shujaa kamili wa klabu hiyo baada
ya Muargentina huyo kutangaza kuondoka klabuni hapo
mwishoni mwa msimu huu.
City wataufanya mchezo wa mwisho dhidi ya West Brom
kuwa wa kipekee kwa Zabaleta kabla ya kutoa mkono wa
kwaheri.

No comments