VIJIMAMBO : HII NDIO PAKA KUBWA DUNIANI.

Omar alikuwa na ukubwa sawa na paka wengine wote
waliokuwa wakiishi pamoja naye, kabla yake kuchukuliwa
na mmiliki wake Stephy Hirst, mwaka wa 2013.


Lakini sasa paka huyu wa aina ya Maine Coon kutoka
Melbourne, Australia ana urefu wa sentimita 120 (futi 3,
inchi 11) na huenda akawa ndiye paka mrefu zaidi duniani
aliyefugwa.
Baada ya sifa zake kuenea mitandaoni, Hirst anasema
Guinness World Records waliwasiliana naye na kumuuliza
kipimo cha paka wake.


Anayeshikilia rekodi kwa sasa ni paka aina ya Maine Coon
kutoka Wakefield, West Yorkshire aliye na urefu wa
sentimita 118 (futi 3, inchi 10.59).
Hirst alianza kuchapisha picha zake Omar kwenye
mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita na moja kati ya
picha hizo ilisambazwa zaidi ya mara elfu 270 katika
mtandao wa kijamii wa Instagram.

No comments