VITUKO : MWANAMKE ALIYE JIOWA BAADA YA KUKOSA MCHUMBA.

Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti
amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa
muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan
ameambia Classic Tv kwamba anaugua ugonjwa huo lakini
hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba
angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za
harusi nami aliambia Classic tv.
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka
mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo
yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia
kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne
na vito alivyovaa.
Anasema kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha
katika studio lakini yeye akawaambia kwamba anataka
picha sawa na zile za harusi.
Hivyobasi alikodisha gari na kwenda kupiga picha hizo
katika maandhari ya harusi.
''Nilipovalia rinda la harusi nilijawa na hisia mpaka nikahisi
kulia''.
Anasema kwamba alihisi kana kwamba ameafikia ndoto
yake ya miaka mingi.
Kwa sababu yeye huugua saratani ya matiti hulazimika
kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano
mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.
Anaongezea kwamba kwa muda mrefu hakuweza
kusimama kwa miguu miwili na kuvaa suruali ndefu,
''nilikuwa nikitembea kwa kiti cha magurudumo''.
Anasema kwamba hakuweza kutembea na kwamba nywele
alizo nazo sio nywele zake asilia.
Habari ya mwanamke huo imewagusa watu wengi
ulimwenguni.
Anasema kwamba anatumia habari yake kuwapa moyo
wanaougua kwamba maisha sio mabaya sana.
''Mbali na maisha na kifo mambo mengine yote ni
madogo''.
Anasema kwamba watu wengi wanaougua huwa na
wasiwasi wataishi kwa muda gani na lini watafariki ama
iwapo matibabu wanayopata yanafanya kazi.
''Lakini mimi nawashauri kwamba usiwe na wasiwasi kwa
sababu hujui, kwa hivyo kwa nini usijiliwaze''?

No comments