SOKA : TIMU YA WASICHA ILIYO FUNGA YA WAVULANA HISPANIA.

Timu ya kandanda ya wasichana nchini uhispania
imeibuka washindi katika ligi ya wanaume licha ya
kutokuwepo uungwaji mkono kwa wanawake wacheza
kandanda nchini humo.

Timu hiyo ya AEM Lleida girls ishinda ligi ya pili ya
wanaume kwa kushinda mechi 21 kat ya 22 ilizocheza.
Mechi za kandanda zinazojumuisha jinsia zote uruhusiwa
nchini Uhispania hadi wachezaji watimie miaka 14, na
wasichana hawa wamecheza na wanaume tangu mwaka
2014.


Hata hivyo hakuna ufadhili kwa timu yoyote ya wanawake
hadi mwaka uliopita na hata klabu maarufu nchini humo ya
Real Madrid haina timu ya wanawake.
"Kuwawezesha wasichana hawa, tulihisi kuwa walistahili
kucheza dhidi ya wavulana kwa sababu unahitaji wapinzani
walio na uwezo ili kuweza kufanikiwa," mkurugenzi wa
AEM Lleida Jose Maria Salmeron alisema.

No comments