HUU NDIYE MWANAMKE MZURI DUNIANI.


Kwa ufupi
Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye
stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili
mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa
mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.
Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu,
lakini ukweli utabaki palepale kwamba kitu au mtu hadi
kuonekana mzuri, lazima kiwe kimekubalika na watu
wengi.
Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na
Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani. Hiyo
imesababishwa na umaarufu walionao walimbwende hao.
Lakini, umaarufu siyo kigezo cha kuwa mzuri kwani wapo
watu wazuri mno na hawatambuliki, kwa sababu tu hawana
umaarufu kama ilivyo kwa Angelina Joliea au Aishwarya
Rai.
Miongoni mwa watu hao ni Fathima Zohar Godabari, raia
wa Saudia Arabia, anayesadikiwa kuwa mwanamke
mrembo kuliko wote walio duniani kwa sasa.
Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye
stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili
mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa
mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.
Mwonekano wa sura yake, urefu na wembamba wa
wastani unatosha kudhihirisha mvuto wa hali ya juu alionao
Fathima. Rangi ya ngozi, uzuri wa nywele na midomo yake
inatosha kueleza na kukubali kuwa ndiye mrembo zaidi
duniani kwa sasa.
Mrembo huyu anatoka katika familia ya kifalme ya nchini
Saudi Arabia akitajwa pia kuwa mstari wa mbele kushiriki
katika masuala yenye manufaa kwa wanawake.
Godabari pia ni mwanaharakati anayejihusisha na utetezi
wa haki za wanawake na mshauri anayewakusanya
wanawake katika makundi madogo madogo kwa lengo la
kujisimamia na kupingana na aina yoyote ya ukatili dhidi
yao.
Licha ya urembo na moyo wa kujitolea alionao, Godabari
anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wanawake wachache
kutoka nchi za kiarabu waliofanikiwa kupata kiwango cha
juu cha elimu.
Kwa hivi sasa yuko nchini Uingereza ambapo anachukua
shahada ya uzamili katika masomo ya uongozi wa
biashara.
Historia kwa ufupi
Fathima Zohar Godabari alizaliwa Oktoba 22,1986 nchini
India. Kwa sasa amefunga ndoa na Sheikh Awadi Al
Muhammad wa ukoo wa kifalme nchini Saudia Arabia.

Imeandaliwa na Isaac Classic

1 comment: