SOKA : Afrika yapewa nafasi ya 9 kwa kombe la Dunia.

Baraza la shirikisho la soka duniani Fifa limeidhinisha
mpango wa kulipatia bara la Afrika nafasi 9 wakati kombe
la dunia litakapoongeza timu zitakazoshiriki katika
kinyanganyiro hicho na kufikia 48, 2026.
Hatua hiyo ilithibitishwa siku ya Jumanne mjini Bahrain.
Kwa sasa bara hilo lina nafasi 5 pekee.
Taifa la kumi la Afrika litashiriki katika mchuano wa
muondoano utakaojumuisha mataifa sita ili kuamua
kuhusu nafasi mbili.
Baraza la Fifa lilipendekeza vile litakavyotoa nafasi hizo 48
mnamo tarehe 30 mwezi Machi.
Kinyang'anyiro hicho kipya kitashirikisha timu 16 kutoka
Ulaya.
Wanachama wa Fifa walipiga kura mnamo mwezi Januari
kuongeza timu zitakazoshiriki kutoka 32 hadi 48 kuanzia
dimba la mwaka 2026.

No comments