News: HATIMAE FIZZO, THITY LOVE KATIKA JUKWAA MOJA, KOOK-K KIJICHO UPANDE

Hii ilikua baada ya masanii wa kike Thity Love kubandika status yake kabambe kwenye ukurasa wake wa FACEBOOK

(KIRUNDI) 

"MY LOVE, NAGERAGEJE GUHISHA ARIKO VYANANIYE, NDUMVA UMUTIMA WANJE UGIRA UPASUKE KUBWURUNDO NKUKUNDA, NDAKWINGINZE UNYEMERERE MVUGE COMBIEN DE FOIS JE T'AIME. SIJE NZOBONA LE 30/04/ HARAGEZE UZUSHIKIRE UMUTIMA WANJE URUHUKE, TU ME MANQUES TELLEMENT, ON S'AIME COMME DE FOUS."

(KISWAHILI) 

< MPENZI WANGU, NIMEJARIBU KUFICHA ILA NIMESHINDWA, NAJIHISI MTIMA KUPASUKA, YOTE SABABU NAKUPENDA, NAKUOMBA UNIKUBALIE NISEME JINSI GANI NINAVYO KUPENDA, NATAMANI TAREHE 30/04/ IWADIE ILI ROHONYANGU ITULIE.
NAKUMISS, TUNAVYOPENDANA KAMA MACHIZI.>




Post hii ilivunja Vichwa vya habari vingi hapa nchini katika vyombo vya habari tofauti. Watangazaji na waandishi wa habari wengi wamemtafuta msanii huyo
na msanii huyo akaongea mambo tofauti, mara eti ni ndoto... Katika Tv show ya Platform aliweza ku funguka na kusema kama kila alichoandika ndivyo mambo yalivyo bila chenga, akimaanisha ni ukweli yeye  na fizzo wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Tarehe 28/04/ mida ya saa 5 asubuhi, katika mkutano wa waandishi wa habari (PRESS CONFERENCE) na msanii huyo gwiji la muziki wa +257 MUGANIGANI FIZZO, alipo ulizwa na mmoja kati ya watangazaji kuhusiana na habari hizo alikanusha kumfaham msanii mwenzie ambae ni Thity love na kuonesha kwamba hajafurahishwa na habari hizo.

Chaajabu ni kwamba jana tarehe 6/04/ mkowani RUMONGE katika tamasha lao wamepanda pamoja jukwaani na kufanya marudio ya wimbo INDORO huku picha zikizagaa mitandaoni wawili hao katika pozi ambalo kila mmoja akiliona lazima agune.


Kwa muujibu wa kipindi cha UKWAJU257 cha Classic Fm, Thity love amefunguka na kusema: " NIKAWAIDA SABABU TUPO KAZINI, WALA HAMNA LAZIADA, FIZZO NI KAKA YANGU NA MIMI NI DADA YAKE." alisema Thity Love

Kauli za msani huyo zimetuacha njiapanda.
"POST ILE ILIKUA KUTAFUTA TU KIKI, WANGU NI KOOK-K." aliendelea kusema Thity love.

Swali ni kwamba Kook K na thity love bado wako pamoja kimapenzi?

Methali ya leo: "MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI."

No comments