SOKA : Hull City yalimwa mabao 4 na kutupwa nje ya Ligi .

Hull City waliondolewa kutoka Ligi ya Premier wakiwa na
mecchi moja ya kucheza kufuatia kipigo kikali
walichopewa na Crystal Palace.
Kikosi hicho cha Marco Silva kilipigwa na mshutuko na
bao la dakika mbili na sekunde 11 baada ya kuanza kwa
mechi.

Mlinzi raia wa Italia Andrea Ranocchia alishindwa kuondoa
mpira eneo la hatari hali iliyompta fusra Wilfried Zaha
kutikiza wafu wa Hull City.
Bao la pili la Christian Benteke lilitimiza mabao mawili ya
Crstal Palace huku mabao mengine mawili yakifungwa na
Luka Milivojevic, na Patrick van Aanholt.
Sasa Hull watajiunga na Sunderland pamoja na
Middlesbrough kusubiri msimu unaokuja.

No comments