Mkuu wa kampuni inayounda simu za bei nafuu India akamatwa
Isaac Classic Bdi
Mkurugenzi wa kampuni ya Ringing Bells, kampuni ya India ambayo imedai kwamba inauza simu ya bei nafuu zaidi duniani, amekamatwa kwa madai ya ulaghai.
Mohit Goel alikamatwa baada ya kampuni moja inayosambaza simu hizo kwa wauzaji kudai kwamba ilikuwa haijapokea simu ambazo ilikuwa imelipia.
Simu hiyo ya Freedom 251, ambayo bei yake ni rupia 251 ($3.70; £3), ilianza kuuzwa Februari 2016.
Lakini ingawa wateja wengi walipokea simu walizoagiza, Ringing Bells imedaiwa kutotimiza maombi yote ya ununuzi wa simu hizo.
Kampuni ya Ayam Enterprises, imesema ililipa rupia 3m ($45,000; £35,800) baada ya Bw Goel kuishawishi ifanye biashara ya kusambaza simu hizo.
Post a Comment