SOCCER: HIRIZI YA BARCELONA

Buba Kelvin Zehot




Sababu nyingi zitatajwa kufuatia kipigo cha Barcelona dhidi ya Deportivo La Coruna, PSG ikiwa mojawapo, lakini ukweli ni kwamba waliikosa hirizi yao.

 Wachezaji kama Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wamekuwa watu muhimu katika kikosi cha Barcelona kwa sababu ya umahiri wao mkubwa katika soka na ufundi wa kuuchezea mpira. Ni wachezaji muhimu katika safu ya mashambulizi ya Barca kama mashine.





 Ikiwa mmoja wao anakosekana, mfumo mzima unayumba, lakini hilo si tatizo kubwa.

Wachezaji wote waliotajwa hapo juu wamecheza na bado Barcelona ilifungwa mechi kadhaa msimu huu. Hirizi ya kweli ya kuihakikishia ushindi Barca, hata kama asipofunga goli lakini uwepo wake uwanjani una faida kwao. Kwa Barcelona mchezaji huyo si mwingine zaidi ya beki wa kati Samuel Umtiti.
Mara zote Mfaransa huyo anapokuwa kwenye kikosi cha Barcelona, huwa wanashinda.
Namba hazidanganyi, uwepo wa Umtiti kwenye kikosi cha Barcelona mechi za La Liga msimu huu umekuwa na tija.





Tupilia mbali idadi ya magoli. Goli lake si muhimu sana kwani timu imesheheni washambuliaji hatari ambao kila mmoja anatamani kuwatazama wakisakata kabumbu dimbani.
Umtiti amecheza mechi 16 za ligi kwenye timu ya Barca msimu huu na katika kila mechi wameshinda. Hakuna sare, wala kufungwa, Barcelona wameshinda pointi tatu katika kila mechi aliyocheza Umtiti, iwe kikosi cha kwanza au ametokea benchi.
Bila ya Umtiti, Barcelona wanasambaratika vipande-vipande. Wameshinda mechi mbili tu katika mechi 11 bila ya beki huyu. Sita kati ya mechi hizo zilikuwa sare, wakati tatu waliambulia kipigo.
Hakuna ubishi hapa, Umtiti ndiye hirizi ya mafanikio ya Barcelona.

Video: Magoal yote ya Barcelona Vs P.S.G  (6-1)




No comments