News: KEBBY BOY KWENYE MAARIFA

Mwanamuziki KABEZA YUSUPH Kebby Boy a.k.a Mnyama pori

Katika shamra shamra za ku sherehekea siku kuu ya uhuru atakua nchini RWANDA ku tumbwiza katika tamasha kabambe SUMMER EVENT tarehe 1, 2 na 3 mwezi Julai, Hii ni moja kati ya fursa kubwa ambayo wanamuziki wengi hutegemea na zamu hii imekuja kwake Kabeza Yussuf.

Nje ya hapo, Kwa muujibu wa Usimamizi wake (Management) BIG GUNZ Entertainment wameweza kufunguka na kusema kwamba wanatarajia ku achia nyimbo mbili za video kwa mkupuo, moja kati ya nyimbo hizo wameshirikiana na msanii kutoka nchini humo RWANDA ambae ni Brice Melody Video hiyo imesimamiwa na muongozaji kutoka nchini humo, ila audio imetengenezwa nchini UGANDA.

Tukumbuke kuwa Kebby Boy mwaka jana alikuja kwenye vichwa vya habari vingi hapa nchini baada ya kuachia wimbo wake SINALAWAMA ambao umesimamiwa na muongozaji MSAFIRI kutoka nchini Tanzania. Mashabiki wa muziki wa Burundi wanasubiri kwa hamu kubwa na shauku kuona ni kitu gani kebby boy ataweza ku kifanya katika nyimbo hizi zijazo.

No comments