NEWS : SOKA ,ZINEDINE ZIDANE NA MKATABA MPYA.

Kocha mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameafikiana
na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba
mpya wa miaka mitatu.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa
mwenye miaka 45 alikuwa mkufunzi wa Timu B ya Real
kabla ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Januari 2016
ambapo ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili
na taji la La Liga mara mbili.

Real watacheza dhidi ya Barca siku ya leo (Jumapili)
mwendo wa saa tano usiku masaa ya Afrika Mashariki
huku mechi ya marudiano itachezewa Bernabeu Jumatano
saa sita saa za Afrika Mashariki.


No comments