Man United wamekubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Hull City
Kelvin Zehot Bdi
Usiku wa January 26 2017 kocha Jose Mourinhoalikiongoza kikosi chake cha Man United kuingia katika uwanja wa Kingston Communicationsunaotumiwa na Hull City kucheza mchezo wao waEFL Cup.
Man United wakiwa ugenini licha ya kuwa na kikosi chao kikiwa na staa ghali zaidi duniani Paul Pogba, walijikuta wakipata kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Hull City, licha ya Paul Pogba kuisawazishia goliMan United dakika ya 66, baada ya Tom Huddlestone kuifungia Hull City goli la uongozi dakika ya 36.
Dakika ya 85 ilikuwa mbaya kwa Man United baada ya El-Hadji Baye Niasse kuifungia goli la ushindi Hull City, licha ya Man United kuwa na wachezaji wao nyota kama Paul Pogba na Rashford hawajafanikiwa kuinusuru Man United na kipigo licha ya kuwa wamefuzu kucheza fainali dhidi ya Southamptonwaliyowatoa Liverpool.
Post a Comment