HATIMAE DORTMUND YAMSAJILI ALEXENDER ISAK
Zehot Kelvin Bdi
Club ya soka ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imefanikiwa kuishinda Real Madrid katika mbio za kuwania saini ya kinda mahiri kutoka Sweden Alexander Isak.
Alexander Isak mwenye umri wa miaka 17 amesajiliwa na Borussia Dortmund akitabiriwa kuja kuwa na umahiri kama mkongwe wa Sweden anayeichezea Man United (Zlatan Ibrahimovic),
Alexander Isak anaripotiwa kusajiliwa kwa dau la pound milioni 8.6 na mkataba wake japo haijatajwa ni wa miaka mingapi, imeripotiwa ni wa muda mrefu.
Gazeti la Marca la Hispania liliripoti kuwa star huyo aliyekuwa asajiliwe na Real Madrid mwishoni mwa wiki hii kwa dau la pound 8.6, anatajwa kuwa ndio mchezaji ghali zaidi kinda kwa Sweden kusajiliwa baada ya Zlatan Ibrahimovic kusajiliwa na Ajax mwaka 2001 akitokea Malmo kwa pound 7.5.
Shuhudia Alexender Isak Ndani ya Dortmund
Post a Comment